KUHUSU JM Brands
KUNA WAKATI MWINGI SANA UTAWASIKIA VIJANA WAKILALAMIKIA SUALA LA UKOSEFU WA AJIRA, LAKINI UBUNIFU KAMA HUU WA JOHN MTATIFIKOLO, NDIO UNAOHITAJIKA ILI AJIRA ZIONGEZEKE.
JOHN NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA, MOSHI, AKISOMEA ELIMU YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (I.T)

MOJA YA UBUNIFU WA JM BRANDS.
JM Brands ni nembo inayojihusisha na ubunifu wa mavazi kwa kila rika kwa mitindo tofauti ya kisasa na kitamaduni.
Aidha nembo hii inafanya kazi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kuprinti fulana mbalimbali, uchoraji wa ramani za majengo, usafirishaji, pamoja na masuala ya urembo na afya.
JOHN, mmiliki wa nembo hii anasema kuwa, JM Brands zamani ilijulikana kama NGONGOTI THE BRIGHT SPARKS na ilianza rasmi kazi zake mnano mwaka 2013, ingawaje kazi hii ya ubunifu aliianza siku nyingi zilizopita.
Vilevile, JOHN alipoulizwa kuhusu mafanikio aliyowahi kuyapata, alisema kuwa, anamshukuru Mungu kwa maana kila anapotambulisha kazi zake anakubalika, kitu ambacho yeye anakichukulia kama moja ya mafanikio kwake.

John anasema kuwa, moja ya changamoto anazokutana nazo ni pamoja na yeye kuwa ndio kwanza anaanza (underground), jambo ambalo kwa sasa linamfanya asitiliwe maanani kimawazo na hata mapokeo kwenye jamii kuwa finyu, likichukua pia muda mrefu kueleweka.

Vilevile, JM Brands inaahidi kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii, ikiwamo kujihusisha na kuwainua vijana wadogo wanaotaka kuinuka kupitia ubunifu wa mavazi.
Kwa sasa JM Brands haijapata mfadhili wa kuiinua, jambo ambalo linaifanya isikuwe kwa haraka, kama yalivyo matarajio ya John, ambaye ndiye mmiliki wa nembo hii.
Katika mahojiano na BLOG HII YA PRINCE BEWISA, John alisema kuwa, miungoni mwa watu anaowatazama kwa sasa kama kioo chake, ni wabunifu kama MUSTAPHA HASSANALI, ALLY REMTULLAH, MANJU MSITA, KHADIJA MWANAMBOKA na wengine wengiambao wakati mwingine hawapo hata kwenye urembo na ubunifu wa mavazi.

John anasema, "USIACHE KIPAJI CHAKO KIONDOKE, KIPAJI NDIYO MTAJI WA KWANZA AMBAO MWENYENZI MUNGU AMEMTUNUKU MWANADAMU. HAIJALISHI NI CHANGAMOTO GANI UNAZOPITIA, ONGEZA BIDII NA IPO SIKU JAMII ITAKUELEWA, KISHA ULIMWENGU, NA HAYO NDIYO MAFANIKIO HUSIKA."
Pia John anaiambia jamii isubiri mambo mazuri yenye kufurahisha na kutia moyo. Hata hivyo aliongeza kuwa, jamii itarajie ubunifu yakinifu wenye kuendana na mazingira na matakwa ya kila mwanajamii husika.
JOHN ALIMALIZIA KWA KUSEMA KUWA ANAWAPENDA WATU WOTE, NA HAIJALISHI NI KWA KIASI GANI WANAMUUNGA MKONO KATIKA KAZI ZAKE.
ANAONGEZA KWA KUSEMA, "UPENDO NI UPENDO, NA NIPO KIUWAJIBIKAJI KATIKA KUUTEKELEZA, NA HILO NALITAMBUA."
John aliongezea kwa kuweka mawasiliano yake kama ifuatavyo;
SIMU: +255659915585 | +255688838637
No comments: